• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Siasa ya kifedha chanzo muhimu cha pengo la kisiasa na kijamii nchini Marekani

    (GMT+08:00) 2019-12-26 18:09:43

    Taasisi ya utafiti wa haki za binadamu ya China leo imetoa makala yenye kichwa cha "siasa ya kifedha yaonesha ukosefu wa demokrasia nchini Marekani", na kudhihirisha kuwa siasa ya kifedha ni sababu muhimu ya pengo la kisiasa na kijamii nchini humo.

    Makala hayo inasema, katika miaka ya hivi karibuni, nchini Marekani ushawishi wa matajiri kwa mambo ya kisiasa umeendelea kuongezeka, huku ushawishi wa watu maskini ukipungua siku hadi siku. Kauli ya "Fedha ni maziwa ya siasa", imefichua ukweli wa mambo ya siasa ya Marekani, ambako imedhihirika kuwa fedha ni muhimu katika mchakato mzima wa kisiasa, na hali hii imekuwa ugonjwa sugu kwa jamii ya nchi hiyo.

    Siasa ya kifedha imeufanya uchaguzi uwe mchezo wa matajiri. Tangu kuanza kwa karne hii, gharama za uchaguzi mkuu wa Marekani ziliongezeka kutoka dola milioni 700 kwa mwaka 2004 hadi bilioini 2 kwa mwaka 2012. Mwaka 2016, gharama za uchaguzi mkuu wa Marekani zilifikia dola bilioni 6.6, ambayo ni nyingi zaidi katika historia ya nchi hiyo.

    Mbali na hayo, fedha nyingi za kisiri pia zimeingia kwenye uchaguzi wa Marekani. Tovuti ya habari ya Shirika la Utangazaji la Marekani iliripoti kuwa, mashirika yasiyotafuta faida hayatahitajika tena kuripoti kwa wizara ya fedha ya Marekani kuhusu chanzo cha fedha zao yaliyochangia kwenye uchaguzi.

    Makala hiyoinaona kuwa, matokeo ya siasa ya kifedha nchini Marekani ni mabaya, kwani imenyima haki ya kisiasa ya raia wa kawaida, na viti vya juu vya serikali vinachukuliwa na matajiri. Hii ni njia ya wazi ya kuwapatia matajiri maslahi ya kijamii, na pia imeongeza ugumu wa kutatua masuala ya kisiasa na kijamii kama vile vitendo vya kimabavu vya kutumia silaha.

    Aidha, makala hiyo imesema, Marekani haiwezi kuepuka siasa ya kifedha kutokana na mfumo wake wa demokrasia ya kibepari. Mfumo huo unaonesha nia ya mabepari, kwamba fedha ni mwanzo na mwisho wa mnyororo wa mambo ya siasa ya Marekani. Wagombea wa vyama tofauti ni wawakilishi wa makundi tofauti ya kibepari.

    Makala hiyo imesisitiza kuwa, siasa ya kifedha imeonesha ukweli wa jamii ya Marekani, ambayo siku zote inajiona ni mfano wa kuigwa wa demokrasia na haki za binadamu, lakini siasa ya kifedha imedhihirisha kuwa huu sio ukweli. Fedha ni msingi wa siasa ya Marekani, ukikosa fedha, ushiriki katika mambo ya kisiasa ni maneno matupu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako