• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • IMF yaipa Ethiopia dola bilioni 2

  (GMT+08:00) 2019-12-26 20:00:13

  Shirika la fedha la Kimataifa (IMF) limesema litaunga mkono mpango unaoendelea wa mageuzi ya uchumi wa Ethiopia ambao unalenga kumaliza kukosekana kwa usawa wa uchumi na kuweka msingi wa ukuaji endelevu na shirikishi.

  IMF, ambayo iliidhinisha mipango ya ufadhili wa dola bilioni 2.9 kwenda Ethiopia mwishoni mwa juma lililopita, ilisema kwamba msaada huo unakusudia kusaidia Mpango wa Marekebisho ya Uchumi.

  Kulingana na IMF, mpango huo, pia utasaidia kupunguza upungufu wa fedha za kigeni nchini Ethiopia, deni, pamoja na kurekebisha sekta ya fedha na kuongeza uhamasishaji wa mapato ambao utasaidiwa na utoaji wa msaada wa kiufundi na mafunzo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako