• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Iraq aonesha utayari wake wa kujiuzulu wakati wa mzozo wa kisiasa

  (GMT+08:00) 2019-12-27 09:15:13

  Kituo cha televisheni cha Iraq kimeripoti kuwa, rais Barham Salim wa Iraq amesema yupo tayari kuwasilisha ombi la kujiuzulu kwa bunge la nchi hiyo baada kukataa kumteua Bw. Asad al-Eidani kuwa waziri mkuu.

  Rais Salim alisema hayo kwenye barua yake kwa spika wa bunge la nchi hiyo Bw. Mohammed al-Halbousi. Pia amesema uteuzi wa Bw. Al-Eidani haujawaridhisha waandamanaji. Amesisitiza kuwa hatua za kisiasa za bunge lazima zikidhi matakwa ya umma, mahitaji ya usalama na amani ya jamii, na kutekeleza utawala bora unaolingana na matumaini ya wananchi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako