• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wakimbizi 1,400 wa Syria warejea kutoka Lebanon

  (GMT+08:00) 2019-12-27 09:16:42

  Gazeti la Syria Elnashra limeripoti kuwa, wakimbizi takriban 1,400 wa Syria wamerejea nyumbani kutoka sehemu mbalimbali nchini Lebanon. Zaidi ya wakimbizi milioni 1 wa Syria wameandikishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi nchini Lebanon, wakati serikali ya Lebanon ikikadiria kuwa idadi halisi ni milioni 1.5. Wimbi la wakimbizi wa Syria kwenda Lebanon limeathiri vibaya uchumi na miundo mbinu nchini humo, na kusababisha maofisa wa Lebanon kuhimiza jumuiya ya kimataifa kutoa msaada katika kuhakikisha wakimbizi wanarudi makwao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako