• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Marefa watakaoichezesha Tanzania dhidi ya Uganda kufuzu kombe la dunia wanawake U20 watajwa

  (GMT+08:00) 2019-12-27 10:13:55

  Mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia Uganda dhidi ya Tanzania kwa Wanawake chini ya umri wa miaka 20 utachezeshwa na Waamuzi kutoka Burundi. Mchezo huo utachezwa kati ya Disemba 31, 2019, Januari 1, na 2, 2020 nchini Uganda, na kuchezeshwa na mwamuzi wa katikati Darlene Nduwayo ambaye atasaidiwa na Fides Bangurambona na Alida Iradukunda. Mwamuzi wa akiba atakuwa Aline Umutoni wakati Kamishna wa mchezo Tesfaneshi Woreta yeye anatokea Ethiopia. Mchezo wa marudiano utachezwa Tanzania kati ya Januari 17, 18 na 19, 2020 na utachezeshwa na Waamuzi kutoka Kenya. Aidha Waamuzi kutoka Kenya pia watachezesha mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia baina ya Tanzania na Burundi Wasichana chini ya umri wa miaka 17.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako