• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Philippe Coutinho kutimkia Ligi Kuu England endapo Bayern Munich watagoma kumchukua jumla

  (GMT+08:00) 2019-12-27 10:14:25

  Nyota wa Kibrazili, Philippe Coutinho amefungua milango ya kurudi kwenye Ligi Kuu England mwakani kama Bayern Munich watagoma kumchukua moja kwa moja wakati muda wake wa mkopo utakapomalizika. Barcelona wamempeleka Coutinho kwa mkopo huko Bayern Munich kwa msimu mzima huku kukiwa na makubaliano ya kumbeba jumla kama watapendezwa naye itakapofika mwisho wa msimu. Anajaribu kucheza soka ya kiwango cha juu kuwashawishi Bayern ili kufungua pochi kumnasa jumla ambapo bei yake inatajwa kuwa ni Euro 120 milioni. Lakini, wasiwasi uliopo ni kama Bayern Munich watakuwa tayari kutoa kiasi hicho cha pesa kumsajili Mbrazili wakati kuna wachezaji wengine wanaocheza kwenye nafasi kama ya Coutinho wanapatikana kwa bei ndogo zaidi. Kama dili la kubali Allianz Arena litakwamba, ripoti zinadai kwamba Coutinho atafungua milango ya kurudi zake England, huku klabu za Manchester United na Tottenham Hotspur zikionyesha dhamira ya kunasa huduma yake tangu dirisha lililopita la majira ya joto.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako