• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • TUZO: Malkia Strikers yatumai kuchukua tena tuzo ya Timu bora ya mwaka ya wanawake

  (GMT+08:00) 2019-12-27 10:14:58

  Timu ya voliboli ya wanawake ya Kenya, Malkia Strikers inatumai kuchukua tena tuzo ya Timu bora ya mwaka ya wanawake ambayo mara ya mwisho iliichukua mwaka 2016, kwenye tuzo za wanamichezo za Personality of the Year (Soya) za Safaricom zilizopangwa kufanyika mwezi ujao huko Mombasa. Malkia Strikers watakabiliwa na ushindani mkali kutoka timu ya taifa ya soka ya wanawake Harambee Starlets pamoja na timu ya kikapu ya Mamlaka ya Bandari ya Kenya (KPA). Mabingwa wa Shirikisho la Soka la Kenya wa Ligi kuu ya wanawake ya Kenya Vihiga Queens, mbao wameshinda mataji mfululizo, nao pia wanawania tuzo hiyo pamoja na timu ya raga ya Kenya Sevens, Lionesses. Malkia Strikers waliteuliwa kuwania tuzo hiyo baada ya kuishinda Cameroon kwenye hatua ya fainali na kuchukua taji la African Games nchini Morocco. Pia wameshinda taji la mwaka 2015 huko Congo Brazzaville.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako