• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Tamasha la wasanii lapelekea kufungwa kwa uwanja wa Sokoine jijini Mbeya

  (GMT+08:00) 2019-12-27 10:15:20

  Bodi ya ligi Kuu Tanzania imefikia maamuzi ya kuufungia uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kuchezewa kwa mechi zozote za mashindano. Uwanja huo umefungiwa kuanzia jana Disemba 26 2019 kutokana na kuharibika sana sehemu ya kuchezea (pitch) baada ya tamasha la wasanii kufanyika katika uwanja huo siku ya Christmass kitu kilichopelekea kuharibika kwa kukanyagwa kwa nyasi za uwanja huo. Timu za Ligi kuu, daraja la kwanza (FDL) na ligi daraja la pili (SDL) zilizokuwa zinatumia uwanja huo kama wa nyumbani au kituo chake, zimeagizwa kutafuta uwanja mwingine wa kutumia hata mchezo wa Prisons na Yanga uliokuwa umepangwa kucheza hapo leo Disemba 27 hauwezi tena kuchezwa na kuhamishiwa Uwanja wa Samora mjini Iringa..

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako