• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sudan na Sudan kusini yaongeza mkataba wa mafuta hadi mwaka wa 2022

  (GMT+08:00) 2019-12-27 16:24:58

  Sudan Kusini na Sudan wametia saini mkataba wa mafuta ambao umeongezwa muda hadi Machi mwaka 2022. Hii ni kulingana na ripoti ya iliyochapishwa na kituo cha habari cha Suna, kinachomilikiwa na serikali. Mkataba huu uliotiwa sahihi siku ya Jumatatu wiki hii jijini Khartoum, unadokeza kwamba Juba italipa dola 26 kwa kila pipa la mafuta litakalopita katika mabomba ya Sudan na dola 24.1 kwa kila pipa litakopita kwenye mabomba ya kampuni ya Bashayer. Kwenye mkataba huo, Sudan Kusini itaisambazia Khartoum mapipa 28,000 ya mafuta kila siku.

  Akizungumza wakati wa kutia saini makubaliano hayo, waziri wa mafuta wa Sudan Kusini bwana Awou Chuang, alisema kwmaba kuongezwa kwa muda wa makubaliano kutazinufainisha nchi hizi mbili na kupiga jeki uchumi wao. Kwa upande wake waziri Kawi na uchimbaji madini, mhandisi Adel Ali Ibrahim, kutia saini kwa makubaliano kunaashiria umoja na ushirikiano baina ya Sudan na Sudan Kusini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako