• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wananchi waombwa kupanda miti kujikimu kiuchumi.

    (GMT+08:00) 2019-12-27 16:25:24

    Spika wa Bunge la kitaifa nchini Tanzania, Job Ngugai, amewataka wakazi wa mikoa ya kanda ya kati kuanza kuwekeza katika upandaji miti, badala ya kujikita katika kilimo pekee ili kuwasaidia kujikwmaua kiuchumi. Spika aliwasihi wakazi wa mikoa hiyo kuiga wenzao wa mikoa ya Kilimanjaro, Kagera na Mtwara ambao wamezamia upandaji miti ili kujiimarisha kiuchumi.

    Kiongozi huyo wa Bunge aliyasema hayo wakati akizindua miradi ya jumuiya ya kikristo Tanzania (CCT) ya kuwawezesha wanawake kujikwmaua kiuchumi. Spika aliwarai watanzania wa mikoa husika kuachana na kilimo cha kutegemea mahindi pekee, badala yake wajikite kwenye ukulima wa miti, ambao ni wa muda mrefu na utawafaa wao pamoja na vizazi vijavyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako