• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Serikali yatoa nafasi za 40,000 za ajira kwa vijana

  (GMT+08:00) 2019-12-27 16:25:45

  Serikali ya Tanzania imetangaza neema ya nafasi za ajira kwa wahitimu 40,000 wa shahada za fani mbalimbali.

  Hatua hiyo inatokana na agizo la Rais Dk. John Magufuli, ambaye aliagiza vijana wote wenye elimu ya Shahada ya Kwanza waliohitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) "Operesheni Magufuli" kupewa ajira katika taasisi mbalimbali za Serikali.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, usimamizi wa Utumishi wa Umma, Dk. Laurean Ndumbaro, alisema mwaka huu wa fedha Serikali imetenga zaidi ya nafasi 40,000 za ajira katika kada mbalimbali.

  Alisema kuanzia Februari mwakani, wataanza kuajiri rasmi lakini kwa sasa wanaanza kutoa ajira kwa vijana 800 waliohitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT). Alipoulizwa ni nafasi zipi watazipa kipaumbele katika ajira hizo, Dk. Ndumbaro, alisema ni katika nyanja za ualimu na afya ambapo kwa upande wa afya alidai kwamba wataangalia uhitaji katika vituo vipya vya afya pamoja na zahanati.

  Hata hivyo, alitaja sifa za vijana waliohitimu JKT kuwa ni lazima wawe wametumikia kwa kipindi kisichopungua miaka miwili na kwamba wanatakiwa kuwasilisha taarifa zao binafsi, vyeti vya elimu, taaluma na vyeti vya kuhitimu mafunzo ya JKT katika Ofisi ya Rais, kitengo cha usimamizi wa Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia barua pepe.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako