• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China aalika dunia kujionea China katika mwaka 2019

    (GMT+08:00) 2019-12-27 17:06:25

    Rais Xi Jining wa China amehudhuria mikutano minne ya kimataifa iliyofanyika nchini China, na shughuli zaidi ya mia moja za pande mbili au pande nyingi, na kufanya ziara saba katika nchi za nje katika mwaka huu. Kutokana na kukabiliwa na mabadiliko makubwa ambayo hayajatokea katika miaka 100 iliyopita, rais Xi amesema, hakuna nchi yoyote inayoweza kutatua masuala yote, na kufungua mlango na kufanya ushirikiano ni njia pekee sahihi. "Mipango ya China" iliiwezesha dunia kuelewe zaidi hali ya China, na pia kupata manufaa mbalimbali halisi.

    Tarehe 6 mwezi Novemba mwaka huu, rais Xi alipokutana na mwezake wa Ufaransa Emmanuel Macron aliyekuwa ziarani nchini China, alisema zikiwa nchi wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na wawakilishi wa ustaarabu wa mashariki na magharibi, nchi hizo mbili zinapaswa kubeba majukumu mengi zaidi, kuinua zaidi kiwango cha uhusiano kati yao, na kuendelea kuongoza kwa kuwa na uhusiano mzuri kati ya nchi kubwa. Viongozi wa China na Ufaransa walitembeleana wakati nchi hizo zikiadhimisha miaka 55 tangu zianzishe uhusiano wa kibalozi, walisisitiza kuwa zikiwa na uhusiano wa wenzi wa kimkakati kwa pande zote , na kuwa nchi kubwa zinazowajibika, China na Ufaransa zitatoa mchango chanya zaidi kwa amani, utulivu na maendeleo ya dunia.

    Tarehe tano mwezi Novemba, rais Xi akihutubia ufunguzi wa maonesho ya pili ya kimataifa ya bidhaa zinazoagizwa na China kutoka nchi za nje, aliwakaribisha watu wa nchi nyingine kutembelea China, ili kujionea soko lake kubwa.

    Kwa nyakati tofauti, Rais Xi pia alikutana na wajumbe wa wageni waliohudhuria maonesho hayo, kongamano la uchumi wa uvumbuzi, na kongamano la kimataifa la Congdu. Alisema sera ya mageuzi na kufungua mlango iliyotekelezwa kwa miaka 40 imeiwezesha China kujiamini. Kufanya mageuzi na kufungua mlango ni njia ya lazima ya China, na China itashikilia njia hiyo daima, bila kujali changamoto na vizuizi vilivyowekwa na wengine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako