Kocha msaidizi wa Gor Mahia Patrick Odhiambo amesema anaamini kuwa timu yake itapata ushindi dhidi ya Posta Rangers katika mchezo wa Ligi Kuu Kenya (KPL) utakaochezwa jumapili, licha ya kocha mkuu wa timu hiyo Steven Polack kuwa mapumzikoni. Odhiambo amesema anaamini timu yake itapata ushindi dhidi ya Rangers inayofunzwa na Sammy Omollo, hivyo kuongeza nafasi yake ya uongozi wa Ligi hiyo kwa pointi tatu. Polack anatarajiwa kurudi Kenya jumatatu ijayo kuendelea na majukumu ya kukinoa kikosi hicho maarufu kama K'Ogalo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |