• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri wa Korea Kusini asisitiza haja ya makubaliano ya muda katika mazungumzo ya nyuklia kati ya Marekani na Korea Kaskazini

  (GMT+08:00) 2019-12-27 18:21:20

  Waziri wa Muungano wa Korea Kusini Kim Yeon-chul amesisitiza haja ya makubaliano ya muda ya mazungumzo ya kuondoa silaha za nyuklia kati ya Korea Kaskazini na Marekani, kama sehemu ya juhudi za kudumisha kasi ya mazungumzo hayo.

  Kim amesema hayo leo wakati alipokutana na waandishi wa habari mjini Seol, na kuongeza kuwa makubaliano ya muda ni hatua muhimu ya kufikia makubaliano ya mwisho.

  Mazungumzo ya ngazi ya kikazi kuhusu kuondoa silaha za nyuklia kati ya Korea Kaskazini na Marekani yalifanyika mara ya mwisho Stockholm, Sweden, lakini hayakupata mafanikio yoyote.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako