• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatoa ufafanuzi wa kisheria kuhusu ulinzi wa maslahi ya wawekezaji wa kigeni

  (GMT+08:00) 2019-12-27 18:27:55

  Mahakama Kuu ya China imetoa ufafanuzi wa kisheria unaofaa kwa Sheria ya Uwekezaji wa Kigeni, ikilinga kulinda vizuri zaidi haki halali na maslahi ya wawekezaji wa kigeni nchini humo.

  Ufafanuzi huo umeelekeza kuwa, mahakama nchini humo hazitaziunga mkono pande zinazodai kuwa makubaliano ya uwekezaji yaliyofikiwa katika maeneo ambayo hayako kwenye orodha hasi ya China ya uwekezaji wa kigeni hayakubaliki kwa kuwa makubaliano hayo hayajakubaliwa ama kusajiliwa na mamlaka husika.

  Makamu rais wa Mahakama hiyo Luo Dongchuan amesema, makubaliano ya uwekezaji ambayo hayatimiza masharti ya orodha hasi wakati yaliposainiwa bado yanaweza kukubaliwa, kama orodha hiyo itapunguza vizuizi kabla ya hukumu kutokewa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako