• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Idadi ya watu waliofariki katika ajali ya ndege ya abiria nchini Kazakhstan yafikia 15

  (GMT+08:00) 2019-12-27 18:48:37

  Mamlaka ya usafiri wa anga nchini Kazakhastan imesema, idadi ya watu waliofariki katika ajali ya kuanguka kwa ndege imefikia 15.

  Ndege hiyo aina ya Fokker mali ya kampuni ya ndege ya Bek iliyokuwa ikitokea Alma-ata kuelekea Nursultan ikiwa na abiria 100, ilianguka leo alfajiri karibu na Alma-ata. Ndege hiyo ilipotea katika rada majira ya saa 2 na dakika 5 baada ya kuondoka, baadaye ilithibitishwa kuanguka na kugonga jengo moja, lakini haikuwaka moto.

  Waziri mkuu wa Kazakhastan Askar Uzakbaiuly Mamin ameiagiza idara maalumu kufanya uchunguzi kuhusu ajali hiyo, pia amesimamisha safari zote za ndege za kampuni ya ndege ya Bek nchini Kazakhastan.

  Rais wa nchi hiyo Kassym-Jomart Tokayev pamoja na mtangulizi wake Nursultan Äbishuly Nazarbayev wametuma salamu za rambirambi kufuatia ajali hiyo na wameahidi kutoa misaada ya kuhitaji kwa jamaa ya watu waliofariki.

  Rais Tokayev ametangaza kesho kuwa siku ya maombolezo kufuatia ajali hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako