• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Roketi kubwa zaidi ya China Long March -5 Y3 yarushwa

    (GMT+08:00) 2019-12-28 16:18:58

    China imerusha roketi yake kubwa zaidi aina ya Long March -5 Y3 kutoka kwenye kituo cha kurushia vyombo vya anga ya juu cha Wenchan, Kisiwani Hainan.

    Roketi hiyo imebeba satellite ya Shijian-20 yenye uzito wa zaidi ya tani 8, ambayo ni satellite nzito zaidi kuwahi kurushwa na ya kisasa zaidi ya mawasiliano kwa China. Baada ya sekunde 2200 satellite hiyo ilifikia kwenye njia yake.

    Naibu mkurugenzi wa idara ya taifa ya mambo ya anga ya China Bw. Wu Yanhua, amesema urushaji huo umefanikiwa, na mafanikio hayo yameweka msingi wa miradi ya utafiti wa anga ya juu katika siku za baadaye, ikiwa ni pamoja na kuichunguza sayari ya Mars, kurudisha sampuli kutoka kwenye mwezi na kujenga kituo cha anga ya juu cha China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako