• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping aelekeza mwelekeo wa maendeleo ya ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja"

    (GMT+08:00) 2019-12-28 18:13:42

    Mwaka 2019 ni mwaka wa 6 tangu pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" litolewe. Katika miaka 6 iliyopita, China imesaini nyaraka 197 za ushirikiano wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na nchi 137 na mashirika 30 ya kimataifa.

    Mwezi Machi, rais Xi alifanya ziara nchini Italia, ambapo China na Italia zimesaini mkubaliano kuhusu kushirikiana kuhimiza ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Mwezi Novemba, rais Xi alifanya ziara nchini Ugiriki, ambapo nchi hizo mbili ziliafikiana kuhusu ushirikiano kupitia "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

    Hata hivyo, katika mkutano wa 2 wa baraza la ushirikiano wa kimataifa wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" uliofanyika mwezi Aprili mwaka huu, rais Xi alitoa hotuba akitoa mwito wa kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kwa sifa ya juu zaidi. Pia alitangaza hatua tano za kupanua mageuzi na kufungua mlango, ikiwemo kupunguza masharti ya kuwekeza kwa kampuni kutoka nje, kuongeza nguvu katika kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika ulinzi wa hakimiliki ya ubunifu, kuongeza uagizaji wa bidhaa na huduma kwa kiasi kikubwa zaidi, kutekeleza kwa ufanisi zaidi uratibu wa sera ya jumla ya uchumi ya kimataifa na kuweka mkazo zaidi katika utekelezaji wa sera za ufunguaji mlango.

    Katika mwaka huu, kwa mara nyingine tena China imeonyesha nia yake ya kushirikiana na kunufaishana fursa ya maendeleo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako