• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwujiza wa China waharakisha juhudi za kupunguza umaskini duniani

    (GMT+08:00) 2019-12-29 16:50:13

    Mwaka jana China ilifanikiwa kuwasaidia zaidi ya watu milioni 10 kuondokana na umaskini uliokithiri, na mwaka huu China inapanga kutokomeza umaskini. Shirika Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri ya "Mwujiza wa China waharakisha juhudi za kupunguza umaskini duniani".

    Tahariri hiyo inasema mafanikio ya China katika mapambano dhidi ya umaskini yanatokana na chama tawala na serikali ya China siku zote kuweka kipaumbele mapambano hayo katika maendeleo ya uchumi na jamii, yanatokana na msingi imara wa uchumi kufuatia utekelezaji wa sera ya mageuzi na kufungua mlango katika miaka 40 iliyopita, na pia yanatokana na sera nzuri ya kuwashirikisha watu wote kwenye mapambano hayo. Balozi maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia ushirikiano kati ya nchi za kusini Bw. Jorge Chediek amesema, Wachina milioni mia kadhaa wamefanikiwa kuondokana na umaskini, jambo hili ni mwujiza katika historia ya binadamu, na pia limetoa mfano wa kuigwa kwa maendeleo ya dunia.

    Hivi sasa China inasaidia nchi nyingine kupambana na umaskini. Licha ya kutoa uzoefu na mawazo, pia inatoa misaada halisi kwa nchi zinazoendelea bila ya kuweka masharti yoyote ya kisiasa, na kuzisaidia kuongeza uwezo wa kujiendeleza kwa kununua bidhaa zao na kutoa uwekezaji katika nchi hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako