• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • TETESI: Atletico Madrid yaizengea saini ya Edinson Cavani kwenye dirisha la Januari

  (GMT+08:00) 2019-12-30 08:42:16

  Mkurugenzi mtendaji mkuu wa Atletico Madrid, Miguel Angel Gil Marin amesema timu hiyo itaingia sokoni kwenye dirisha la Januari kwa kazi moja tu, kusajili mshambuliaji wa kati. Los Rojiblancos wamekuwa wakihusishwa na mpango wa kumsajili straika wa Paris Saint-Germain, Edinson Cavani. Hata hivyo, Cavani ameripotiwa kwamba amekubali kujiunga na Atletico mwishoni mwa msimu akitaka kumaliza msimu huu akiwa na klabu yake ya PSG. Kama Cavani atakwenda kwenye kikosi hicho cha Atletico basi atakutana na washambuliaji wengine matata Diego Costa na Alvaro Morata. Wakati wakisubiri kunasa saini ya Cavani, Atletico Madrid wamekuwa kawaida yao kuwa na huduma bora kabisa kutoka kwa washambuliaji wa kati bora duniani baada ya mastaa kibao kupita kwenye kikosi hicho.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako