Jumla ya Wanariadha 20 wamechaguliwa kuunda timu ya Taifa watakaoshiriki Michezo ya Olimpiki 2020 nchini Japan. Kwa mujibu wa Katibu wa Shirikisho Riadha Tanzania (RR), Ombeni Zavala, tayari wachezaji hao wameshapewa taarifa na wanatarajia kuingia kambini Januari 5 mwakani ili kuendana na kalenda ya kimataifa. Kiongozi huyo ameweka wazi kuwa hadi sasa ni wachezaji wawili tu wenye viwango vya kushiriki mashindano ambao ni Felix Simbu na Failuna Abdi. Amesema Shirikisho kwa kutambua hilo wameamua kuwaweka mapema kambini wachezaji ili kufikia Juni watakuwa wameshakamilisha utaratibu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |