• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uhusiano kati ya China na Russia waingia kwenye zama mpya

  (GMT+08:00) 2019-12-30 08:58:23

  Mwaka 2019 ni mwaka wa 70 tangu China na Russia zilipoanzisha uhusiano wa kibalozi. Katika mwaka huu rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Russia Vladimir Putin wamekutana mara kwa mara. Wakati wa kukabiliana kwa pamoja na mabadiliko makubwa yanayoendelea kutokea kwenye jukwaa la kimataifa, China na Russia zimechagua kuwa karibu zaidi, ili kuandika historia mpya kwa kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

  Mawasiliano ya karibu kati ya marais wa China na Russia yameleta matunda mengi katika uhusiano kati ya nchi hizo mbili mwaka huu. Mwanzoni mwa mwezi Disemba, rais Xi na rais Putin walishuhudia kwa njia ya video ya moja kwa moja uzinduzi wa bomba la kusafirisha gesi asilia kati ya China na Russia. Mbali na hayo, ujenzi wa "Ukanda mmoja na Njia moja" umeunganishwa na mkakati wa Muungano wa Uchumi kati ya Ulaya na Asia, miradi mikubwa ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili kwenye sekta za anga na anga za juu imeendelea kupiga hatua, lugha ya Kichina imejumuishwa kwenye Mtihani wa Taifa wa Russia, na idadi ya jozi za miji rafiki kati ya China na Russia imefikia 146 na kadhalika.

  Katika mwaka huu unaokaribia kumalizika, waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi ameutaja uhusiano kati ya China na Russia kuwa ni wa karibu zaidi, imara zaidi, uliopevuka zaidi na thabiti zaidi miongoni mwa mahusiano kati ya nchi kubwa. Pia ameeleza imani yake kuwa chini ya uongozi wa pamoja wa wakuu wa nchi hizo mbili, uhusiano huo hakika utaendelea kufungua ukurasa mpya katika historia na kufikia kilele kipya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako