• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wapiganaji 19 wa kundi la Hashd Shaabi wauawa kwenye shambulizi la Marekani nchini Iraq

  (GMT+08:00) 2019-12-30 09:07:49

  Wapiganaji 19 wa kundi la Hashd Shaabi la Iraq wameuawa na wengine 35 wamejeruhiwa kwenye shambulizi lililofanywa Jumapili na jeshi la Marekani kwenye jimbo la Anbar magharibi mwa Iraq.

  Kiongozi wa kundi hilo Jawad al-Rebi'awi amesema mashambulizi hayo yalilenga makao makuu ya brigedi za 45 na 46 karibu na mji wa mpakani wa al-Qaim kwenye mpaka na Syria, na baadhi ya wapiganaji bado wako kwenye kifusi.

  Taarifa iliyotolewa na kituo cha pamoja cha habari nchini Iraq imesema Marekani imefanya mashambulizi matatu dhidi ya makao makuu ya brigedi ya 45 ya kundi hilo. Jeshi la Marekani pia limetoa taarifa likisema limeshambulia kambi tano za kundi la Kata'ib Hezbollah nchini Iraq na Syria, kujibu mashambulizi yanayofanywa na kundi hilo dhidi ya vikosi vya Marekani nchini Iraq.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako