• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Abbas asema hakuna uchaguzi hadi wapalestina watakaporuhusiwa kupiga kura kwenye Jerusalem Mashariki

    (GMT+08:00) 2019-12-30 09:15:03

    Rais Mahmoud Abbas wa Palestina amesisitiza kuwa hakuna uchaguzi mkuu wa Palestina isipokuwa hadi Israel itakapowaruhusu wapalestina kupiga kura kwenye eneo la Jerusalem Mashariki.

    Rais Abbas amesema Palestina haitafanya uchaguzi wowote bila Jerusalem, amesema wakazi wowote wa Jerusalem lazima wapige kura kwenye eneo la katikati ya Jerusalem Mashariki.

    Msimamo wa Rais Abbas wa kushikilia kufanya uchaguzi kwenye eneo la Jerusalem Mashariki ni changemoto kwa tamko la rais Donald Trump wa Marekani alilolitoa mwishoni mwa mwaka 2017 kwamba Jerusalem itakuwa mji mkuu wa Israel.

    Rais Abbas amekataa kutoa agizo la rais kuhusu kuweka tarehe ya kufanya uchaguzi wa wabunge na urais kwenye ardhi ya Palestina, kabla ya kupata ruhusa ya Israel kujumuisha Jerusalem Mashariki katika upigaji kura.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako