• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Leicester yapiga msumari kwenye jeneza la Pellegrini

  (GMT+08:00) 2019-12-30 18:25:02

  Klabu ya Leicester ilitia kikomo enzi ya Manuel Pellegrini kama kocha mkuu wa West Ham baada ya kuilima 2-1 uwanjani London, Jumamosi. Pellegrini aliingia katika mchuano huo akikodolea macho kuachishwa kazi kutokana na msururu wa matokeo duni, na alitimuliwa dakika 10 baada ya mechi hiyo kumalizika. Leicester ilifanyia kikosi chake kilicholipuliwa na Liverpool 4-0 Desemba 26 mabadiliko tisa. Mshambuliaji Jamie Vardy alikuwa katika orodha ya wachezaji walioachwa nje, huku Kelechi Iheanacho na Demarai Gray wakitumia vilivyo fursa nadra ya kuanza mechi ligi kwa kufunga bao moja kila mmoja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako