• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yachukua hatua halisi katika kuboresha usimamizi wa dunia

    (GMT+08:00) 2019-12-30 18:57:01

    Matukio mawili yaliyotokea katika jumuiya ya kimataifa mwishoni mwa mwaka huu, yameleta wasiwasi mkubwa kwa watu. La kwanza ni kuwa kutokana na vizuizi vya Marekani, bodi ya rufaa ya Shirika la Biashara la Kimataifa WTO imekwama kutokana na upungufu wa idadi ya majaji, hivyo mfumo wa biashara ya pande nyingi umeathiriwa vibaya. La pili ni kwamba ingawa mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa uliofanyika huko Uhispania uliongezewa siku mbili zaidi, lakini haukupata maendeleo yoyote. Matukio hayo yanaonekana kutokuwa na uhusiano wowote, lakini uhalisi ni kwamba usimamizi wa dunia unakabiliwa na changamoto kubwa ambazo hazikuwepo awali.

    Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na upinzani wa utandawazi, ongezeko la shinikizo la kushuka linaloukabili uchumi wa dunia, jumuiya ya kimataifa inapokabiliana na changamoto kuu, inashindwa kufikia makubaliano ya pamoja. Chanzo kikuu ni kuwa mfumo wa usimamizi wa uchumi wa dunia hauendani na mabadiliko ya hali ya kimataifa. Pia haufai kwa matakwa ya kuinuliwa kwa hadhi na sauti za nchi zinazojitokeza kiuchumi, uwakilishi na usawa vimekumbwa na upungufu, na baada ya Vita ya Pili ya Dunia, mfumo na kanuni za usimamizi wa dunia zinazoongozwa na nchi za magharibi haziendani na wakati. Wakati huohuo, ili kulinda hadhi ya umwamba, nchi kadhaa za magharibi zinachukua hatua za kushinikiza na kuzuia nchi zinazojitokeza kiuchumi, hata zimekataa kutekeleza majukumu yao ya kimataifa, na kusababisha hali ya usimamizi wa dunia kuzidi kuwa mbaya.

    Katika miaka ya hivi karibuni, kutoka upande wa kulinda haki za kujiendeleza na maslahi za pamoja za jumuiya ya kimataifa, China imeshiriki kwenye mageuzi ya mfumo wa usimamizi wa dunia, huku ikipendekeza mpango wa dhana, mawazo na hatua unaolenga kujenga mfumo wa usimamizi wa dunia wenye mazungumzo, ujenzi na ushirikiano wa pamoja na kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

    Katika mchakato wa kuhimiza mageuzi ya usimamizi wa dunia, China siku zote ni upande unaochukua hatua halisi. Kutoka pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" lililotolewa miaka sita iliyopita, uzinduzi wa mashirika ya kifedha ya pande nyingi ikiwemo Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia, kutimiza malengo ya ahadi ya kupunguza hewa ya kaboni miaka mitatu mapema, na kuhimiza mageuzi ya mashirika ya pande nyingi, China imefanya juhudi halisi kuendelea kutia nguvu kwa maendeleo tulivu ya dunia.

    Jambo jingine linalotakiwa kuzingatiwa ni kuwa China kushiriki na kuhimiza mageuzi ya mfumo wa usimamizi wa dunia hakulengi kuzindua mfumo mpya, bali ni kubuni na kuboresha mfumo uliopo. Lengo hilo limehakikisha pendekezo la China kuweza kuzingatia kwa kiasi kikubwa maslahi ya pande mbalimbali, hivyo linaungwa mkono na jumuiya ya kimataifa.

    Hivi sasa, changamoto zinazoikabili jumuiya ya kimataifa zinazidi kuwa kubwa, matatizo yanayoukabili usimamizi wa dunia yanatakiwa kutatuliwa sasa. China inapenda kufanya juhudi pamoja na pande mbalimbali kuhimiza utaratibu wa kimataifa kuelekea upande wenye haki na usawa zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako