• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa asema vijana ni chanzo kikubwa cha matumaini

  (GMT+08:00) 2019-12-30 20:06:57

  Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa hotuba ya Mwaka Mpya ya 2020 na kusema, dunia inaingia mwaka mpya kwa hali ya kutokuwa na uhakika na utulivu, na vijana kote duniani ndio chanzo kikubwa cha matumaini kwa dunia.

  Katika hotuba yake, Bw. Guterres amesema dunia inakabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo ukosefu wa usawa, kuongezeka kwa vitendo vya chuki, lakini katika hatua ya hali ya hewa, usawa wa kijinsia na haki za binadamu, vijana wapo mstari wa mbele, huku akiongeza kuwa ni muhimu kuwasaidia vijana kuchukua jukumu lao katika kujenga dunia.

  Bw. Guterres ameongeza kuwa, mwakani, Umoja wa Mataifa utatimiza miaka 75 tangu kuanzishwa, na utazindua Mwongozo wa hatua za malengo ya maendeleo endelevu, ambayo ni mpango wa utandawazi mwafaka.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako