• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirika Kuu la Utangazaji la China lachagua habari muhimu kumi za kitaifa za mwaka 2019

    (GMT+08:00) 2019-12-30 20:08:31

    Shirika Kuu la Utangazaji la China limechagua habari muhimu kumi za kitaifa za mwaka 2019.

    1. Shughuli za maadhimisho ya miaka 70 ya Jamhuri ya Watu wa China zilifanyika kwa shangwe kwenye Uwanja wa Tian An Men wa Beijing tarehe 1 mwezi Oktoba, ambapo rais Xi Jinping wa China alitoa hotuba muhimu.

    2. Mkutano wa nne wa wajumbe wote wa kamati kuu ya 19 ya Chama cha Kikomunisti cha China ulifanyika tarehe 28 hadi 31 mwezi Oktoba mjini Beijing, na kufungua ukurasa mpya katika utawala wa nchi.

    3. Wanachama wote wa Chama cha Kikomunisti cha China walipata mafunzo yenye kauli mbiu ya "Kutosahau sababu ya kuanza safari na kukumbuka kwa moyo majukumu yetu".

    4. Uchumi wa China unaendelea kwa utulivu na kuleta maendeleo ya uchumi yenye ubora zaidi.

    5. Shughuli kuu nne za kidiplomasia ikiwemo Baraza la ushirikiano wa kimataifa la "Ukanda Mmoja, Njia moja" zimetoa mchango katika kuhimiza kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja na kutetea utaratibu mpya wa kimataifa.

    6. Mkutano wa kuadhimisha miaka 20 tangu Macau irudi China na sherehe ya kuapishwa kwa serikali ya awamu ya tano ya mkoa wa utawala maalumu wa Macao vilifanyika tarehe 20 mwezi Desemba, ambapo vimeonyesha dhamira imara ya serikali kuu ya China katika kuhimiza sera ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili".

    7. Uwanja mpya wa ndege wa Daxing ulizinduliwa rasmi tarehe 25 mwezi Septemba, ambao umekuwa alama mpya ya ujenzi na uendeshaji wa kituo cha safari za anga cha kimataifa.

    8. Timu ya mpira wa wavu ya wanawake ya China ilitulia kwa mara 11 kwa mfululizo na kupata ubingwa kwenye Kombe la Dunia la mpira wa wavu ya wanawake.

    9. Chombo cha uchunguzi cha anga za juu cha China kinachojulikana kwa jina la Chang'e-4 kimetua upande wa mwezi tarehe 3 mwezi Januari na kuwa chombo cha anga cha kwanza kutua eneo hilo ambalo halijawahi kuonekana duniani, ambacho kimefanikiwa kurudisha picha ya kwanza ya karibu ya upande wa mwezi na kufungua ukurasa mpya katika uchunguzi wa mwezi.

    10. Wizara ya viwanda na mawasiliano ya China iliidhinisha rasmi leseni za teknolojia ya 5G kwa matumizi ya kibiashara tarehe 6 mwezi Juni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako