• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • EPZA ya vutia teknolojia katika viwanda

  (GMT+08:00) 2019-12-30 20:16:58
  Mamlaka ya ukanda maalumu wa Uwekezaji (EPZA) imesema inaendelea kuvutia uwekezaji kwenye viwanda vinavyotumia teknolojia ya kisasa, ili kukuza na kuendeleza wajasiriamali waitumie kukuza uchumi.

  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji wa EPZA, James Maziku alipozungumzia uwekezaji wa kiwanda cha kutengeneza kadi za kielekroniki cha DZ Cards Afrika, kilichopo katika Eneo Maalum la Uwekezaji la Benjamin William Mkapa jijini Dar es Salaam.

  Baadhi ya viwanda vilivyopo katika maeneo maalumu ua uwekezaji wa EPZ ni pamoja na viwanda vya nguo, vinavyochakata nafaka, vifaa vya ujenzi na bidhaa za ngozi.

  Maziku amesema kuongezeka kwa mahitaji ya kadi za kieletroniki na kukuza uchumi usiotumia fedha taslimu, ndio imefanya kiwanda cha DZ Cards Afrika kupanua masoko ili kusambaza bidhaa zake katika bara lote la Afrika.

  Kiwanda cha DZ Cards Afrika kilianza uzalishaji miaka minne iliyopita na tangu wakati huo, kimepata wastani wa mauzo ya dola za marekani milioni 2.9(zaidi y ash bilioni 6.67)

  Maziku amesema kiwanda cga DZ Cards Afrika, kitakuwa na uwezo wa kuajiri zaidi ya watu 400 wakati uzalishaji ukiwa katika kiwango cha juu. Kwa sasa kinaajirei watu takriban 100.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako