• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mauzo duni Krismasi, wafanyabiashara waumia

  (GMT+08:00) 2019-12-30 20:17:37
  Wafanyibiashara walipata pigo baada ya Wakenya kupunguza matumizi ya fedha kwa sherehe za Krismasi mwaka huu, ithibati ya kudorora kwa uchumi.

  Mauzo katika katika maduka makuu na wauzaji wa nguo na vyakula kama vile kuku, yalikuwa duni wakati wa sherehe za Krismasi.

  Kupungua kwa mauzo wakati wa sherehe za Krismasi kunatokea wakati ambapo mashirika mbalimbali yameripoti kupungua kwa mapato huku baadhi ya wafanyakazi wakitimuliwa na waliosalia wakinyimwa nyongeza ya mishahara.

  Serikali ya kitaifa na kaunti pia zimechelewesha malipo ya jumla ya Sh100 bilioni zinazodaiwa na wakandarasi. Baadhi ya wakandarasi wameshindwa kulipa mikopo ya benki hivyo mali yao kupigwa mnada na kusitisha operesheni.

  Kutokana na hilo, takwimu za Benki Kuu ya Kenya (CBK) zinaonyesha kwamba fedha zinazotumiwa na Wakenya nje ya benki zimepungua hadi Sh176.9 bilioni. Hiyo ndiyo mara ya kwanza kwa fedha zinazozunguka miongoni mwa Wakenya, nje ya benki, kupungua kwa kiasi hicho tangu Julai 2015.

  Sekta ya utalii haikusazwa kwani uchunguzi wa Taifa Leo ulibainisha kwamba katika maeneo ya Pwani, kulikuwa na wageni wachache hotelini ikilinganishwa na miaka iliyopita.

  Uchumi wa Kenya ulikua kwa asilimia 5.6 kati ya Januari na Juni, mwaka huu. Katika kipindi sawa mwaka jana uchumi ulikua kwa asilimia 6.4.

  Kutokana na hali ngumu ya uchumi kampuni mbalimbali za kibinafsi zimesitisha shughuli ya kuajiri wafanyakazi wapya.

  Kampuni nyingi zilizoorodheshwa katika Soko la Ubadilishanaji Hisa (NSE) tayari yametoa onyo kuhusu kudorora kwa faida.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako