• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Ronaldo kukimbilia kwenye filamu

  (GMT+08:00) 2019-12-31 16:09:44

  Mshambuliaji hatari wa timu ya taifa Ureno na klabu ya Juventus, Cristiano Ronaldo, ameweka wazi mipango yake na kuwa mwigizaji mara baada ya kustaafu soka. Nahodha huyo wa Ureno, amesema filamu ni moja kati ya vitu ambavyo anavipenda, hivyo haoni sababu ya kushindwa kufanya mara baada ya kutundika daruga. Ronaldo anataka kufuata nyayo za nyota wa zamani wa Manchester United, Eric Cantona, ambaye kwa sasa anafurahia maisha yake mengine ya kucheza filamu mara baada ya kustaafu soka mwaka 1997 akiwa na klabu hiyo. Ronaldo itakuwa rahisi kuingia kwenye filamu kutokana na baadhi ya vitu ambavyo anavifanya na kumuingizia fedha nje ya soka kama vile kufanya matangazo mbalimbali ya mitindo na mambo mengine.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako