• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Ukata wamkimbiza kocha AFC Leopards

  (GMT+08:00) 2019-12-31 16:10:06

  Kocha wa AFC Leopard ya Kenya Casa Mbungo ameondoka klabuni hapo baada ya kusitisha mkataba wake. Kocha huyo Mnyarwanda aliwaaga wachezaji na wafanyakazi wenzake hapo jana, akiwataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii. Inadaiwa kuwa kocha huyo ameondoka kwenye klabu hiyo kutokana na ukata, na pia kutolipwa mshahara kwa miezi mitano huku akiwa anadai malimbikizo ya mshahara wake ambayo ni zaidi ya Sh milioni mbili za Kenya. Kocha huyo ametoa siku 15 kwa klabu hiyo kumlipa madai yake, ikishindikana ataishtaki klabu hiyo kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa, FIFA.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako