• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Samatta, Salah, katika kikosi cha Waafrika waliotisha 2019

  (GMT+08:00) 2019-12-31 16:12:32

  Zikiwa zimebaki saa kadhaa kuumaliza mwaka huu wa 2019, nikufahamishe tu mastaa wa Kiafrika waliofanya vizuri mwaka huu katika ligi mbalimbali za mataifa makubwa barani Ulaya. Nianze na Andre Onana, ambaye licha ya timu yake ya Ajax kuondolewa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, Onana ambaye ni raia wa Cameroon amekuwa katika kiwango bora ndani ya michezo 18 ya Ligi Kuu Uholanzi. Ubora wake unahusishwa na chuo cha FC Barcelona ambacho alipitia kabla ya kutua Ajax Juni 14, 2015. Mwingine ni Serge Aurier, ambaye ni beki wa pembeni wa timu ya Tottenham Hotspurs. Ingawa hajafunga bao hata moja, lakini amesaidia kufungwa kwa mabao matatu katika michezo 15 ya Ligi Kuu England. Ramy Bensebaini ni beki wa kushoto wa Borussia Monchengladbach, na ni raia wa Algeria. Amecheza michezo nane katika Ligi Kuu ya Ujerumani na kufunga mabao matatu na kusaidia bao moja. Mchezaji mwingine ni Joel Matip, raia wa Cameroon ambaye ni mmoja wa walinzi makini wa timu ya Liverpool. Kutokana na kukataa kujiunga na kikosi cha timu ya taifa ya Cameroon katika fainali za Mataifa ya Afrika, Wacameroon wanamchukulia kama msaliti. Sadio Mane naye pia ni mchezaji aliyefanya vizuri katika mwaka huu. Licha ya kucheza kama mshambuliaji wa pembeni, Mane amekuwa hatari kiasi cha kushindana na washambuliaji wa kati katika kuwania kiatu cha ufungaji bora wa Ligi Kuu England. Katika klabu yake ya Liverpool, Mane amefunga mabao tisa na kusaidia mabao nane katika michezo 17 ya Ligi hiyo. Mo Salah ni mchezaji anayeweza kucheza nafasi mbalimbali kama ilivyo kwa Mane. Salah, raia wa Misri, ni mzuri katika kucheza nyuma ya washambuliaji, kumalizia, n ahata kuassist. Ameifungia Liverpool mabao tisa huku akiassist mabao manne katika michezo 14 aliyocheza. Nimalizie na Mbwana Samatta, raia wa Tanzania, ambaye amekuwa katika kiwango bora msimu huu. Ameifungia klabu yake ya KRC Genk mabao saba katika michezo 20 ya Ligi Kuu Ubelgiji.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako