• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Mahakama yaamuru kutopandishwa kwa ada ya maegesho

  (GMT+08:00) 2019-12-31 20:05:54
  Mahakama kuu nchini Kenya imeamuru serikali ya Kaunti ya Nairobi isiongeze ada ya kuegesha magari hadi kesi iliyowasilishwa na shirikisho la watumiaji bidhaa (Cofek) isikizwe na kuamuliwa.

  Jaji James Makau aliamuru kesi iliyowasilishwa na Cofek isikizwe Februari 17, 2020.

  Jaji Makau alisema , kesi hiyo ingelisikizwa Januari 2020 lakini anasikiza kesi nyingine katika mahakama kuu pamoja na majaji wengine wawili zinazohusu masuala ya katiba.

  Akiwasilisha kesi ya Cofek, wakili Henry Kurauka, ameeleza mahakama kwamba wakazi wa Nairobi hawakuarifiwa kama inavyotakiwa kisheria kabla ya kuongeza ada za magari ya wamiliki binafsi na ya kibiashara.

  Ada ya kuegesha gari dogo iliongezwa kutoka Sh200 hadi Sh400.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako