• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Tembo waharibu mimea kasese

    (GMT+08:00) 2019-12-31 20:06:18
    Kundi la tembo limeharibu bustani za mahindi, mashamba ya ndizi na alizeti katika Wilaya ya Kasese nchini Uganda.

    Tembo hao, ambao inaaminika wametoroka kutoka Hifadhi ya Taifa ya Queen Elizabeth Jumanne na Alhamisi, walivamia vijiji vya Rwehingo, Bugemu na Katholhu katika kaunti ndogo ya Nyakiyumbu.

    Wakazi kutoka maeneo yaliyoathirika wanasema wameripoti tukio hilo kwa Mamlaka ya Wanyamapori ya Uganda (UWA) ili kuingilia kati.

    Msemaji wa UWA, Bwana Bashir Hangi, alisema kwa miaka iliyopita, wakulima kwenye eneo hilo wamekuwa wakivamiwa na tembo na kula mazao yao.

    Hata hivyo, alisema sheria mpya ina vifungu vya kulipia fidia watu wanaopoteza mali kutokana na kushambuliwa wa wanyama na porini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako