• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi Kairuki aanika mikakati kuimarisha ushirikiano China, Tanzania 2020

    (GMT+08:00) 2019-12-31 20:12:32

    Na Majaliwa Christopher

    UBALOZI wa Tanzania nchini China umeelezea mipango na mikakati yake ya kuendelea kuvutia wawekezaji na watalii kutoka China pamoja na namna ya kutafuta masoko zaidi kwa bidhaa za Tanzania mwaka 2020

    Uwekezaji wa China nchini Tanzania kupitia kwa Mpango wa Ukanda Mmoja na Njia Moja hadi kufikia kwaka 2018, ulifika Dola za Kimarekani Bilioni 5.77 (takriban Shilingi Trilioni 12.7 za Tanzania).

    Uwekezaji huo umefanyika katika miradi 670 huku ikizalisha jumla ya nafasi za ajira 150,000 katika sekta mbalimbali za uchumi.

    Vilevile, Mwaka Mpya wa 2020, Tanzania na China zinaadhimisha miaka 55 tangu kasainiwa kwa Mkataba wa Urafiki baina ya Nchi hizo mbili.

    Mkataba huo ulisainiwa katika kipindi kigumu cha vita baridi ulimwenguni --ambako ilisemekana kuwa ni jambo la hatari kuwa na mahusiano na Taifa lenye mrengo wa kijamaa.

    Katika taarifa yake ya mahojiano maalum, Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki, nchi hizo mbili zimeweka mipango na mikakati madhubuti kuhakikisha ushirikiano katika sekta mbalimbali za kimandeleo zinaendelea kuimarishwa.

    Balozo Kairuki alitoa Shukrani za dhati kwa wananchi na wadau Serikalini na Sekta Binafsi na vyombo vya habari kwa ushirikiano mkubwa walioutoa katika kufanikisha majukumu mbalimbali ya Ubalozi katika mwaka 2019.

    Alisema kuwa kupitia ushirikiano huo malengo ya kutafuta fursa za mafunzo, uwekezaji, masoko na utalii yalitekelezwa.

    "Katika mwaka 2020 Ubalozi utaendelea kutafuta masoko ya bidhaa za Tanzania, kutafuta teknolojia mbalimbali za uzalishaji, kutafuta fursa za mafunzo (scholarships) katika fani mbalimbali, kuvutia uwekezaji pamoja na kutangaza vivutio vya utalii," alieleza Balozi Kairuki.

    Balozi huyo pia alieleza kuwa katika mwaka 2020, kutakuwa na matukio mbalimbali ya kutangaza utalii katika soko la China na Vietnam.

    Matukio hayo ni pamoja na Tanzania Tourism Roadshow itakayofanyika kwenye mijiji ya Guangzhou, Shanghai, Beijing na Chengdu Mwezi Aprili 2020 na China Outbound Travel and Tourism Market (COTTM Conference) itakayofanyika tarehe 1-3 Aprili 2020.

    Matukio mengine ni Shanghai World Travel Fair itakayofanyika tarehe 23-26 April 2020 pamoja na Tanzania Tourism Roadshow itakayofanyika Jijini Hannoi na Ho Chin Mi mwezi Aprili 2020.

    "Ni matumaini yetu kwamba idadi ya watalii itaongezeka zaidi mwakani kwasababu shirika la ndege la Air Tanzania litaanza safari za moja kwa moja kutoka Dar es salaam kwenda China (Guangzhou).

    Pia kutakuwa na programu maalum ya Chartered flights kutoka China (Hangzhou) kwenda Tanzania kuanzia mwezi Februari 2020," alibanisha Balozi Kairuki.

    Sambamba na hilo, Balozi alielezea matukio mbalimbali katika mwaka 2020 ambayo yanalenga kutangaza bidhaa za Tanzania katika soko la China pamoja na kupata ufahamu wa teknolojia mbalimbali zilizopo China zenye manufaa kwa Tanzania.

    Matukio hayo kwa mujibu wa Kairuki ni pamoja na Awamu ya kwanza ya Maonesho ya Canton Fair yatakayofanyika kuanzia tarehe tarehe 15- 19 Aprili 2020 na Awamu ya Pili ya Maonesho ya Canton Fair yatakayofanyika kuanzia tarehe 15-19 Oktoba 2020.

    Matukio mengine ni pamoja na China International Importation Expo yatakayofanyika tarehe 5-10 Novemba 2020 - ambayo yatakuwa na Mabanda Mawili Maalum ya kuonesha bidhaa za Tanzania ikiwa ni pamoja na bidhaa za kilimo na bidhaa za madini.

    Kw upande wa uwekezaji, Kairuki alieleza kuwa Ubalozi umejipanga kufanya mikutano minne ya kuvutia uwekezaji nchini China.

    "Aidha, Ubalozi utaendelea kutafuta fursa za ufadhili kwa Watanzania kusomea katika vyuo vikuu vya China pamoja na kufafuta fursa za mafunzo kwa vitendo ya wahandisi na Madaktari," alieleza Kairuki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako