• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Uuzaji wa magari mapya wapungua

  (GMT+08:00) 2019-12-31 20:12:59
  Uuzaji wa magari mapya kwa mwaka unaomalizika mwezi huu unakadiriwa kushuka kwa asilimia 8.5 ikilinganishwa na 2018, ikiashiria kipindi kigumu cha biashara kwenye sekta hiyo.

  Takwimu kutoka Chama cha wauza magari magari cha Kenya (KMI) zinaonyesha kuwa wafanyabiashara wakiwemo wa Isuzu East Africa na Toyota Kenya waliuza magari 12,030 katika miezi 11 iliyomalizika Novemba.

  Uuzaji wao kwa mwezi huu unatarajiwa kufikia magari 1,093.

  Utendaji wao bora katika miaka ya hivi karibuni ilikuwa mwaka 2015 wakati mauzo yalifikia magari 19,451.

  Isuzu, ambayo ni muuzaji mkubwa wa magari nchini humo, hata hivyo ilipata ongezeko la mauzo ya asilimia 11.

  Nayo mauzo ya Toyota Kenya, ambayo iko katika nafasi ya pili, yalishuka hadi 3,162 kutoka 3,973 ya kipindi hicho hicho mwaka 2018.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako