• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudani Kusini na Sudan zasaini makubaliano ya kurefusha mkataba wa usafirishaji mafuta

    (GMT+08:00) 2019-12-31 20:13:21

    Sudani Kusini na Sudan zimesaini makubaliano ya kuongeza muda wa makubaliano ya mauzo ya mafuta hadi Machi 2022.

    Shirika la habari la serikali Suna linaripoti kuwa makubaliano hayo, yaliyotiwa mjini Khartoum, yanasema kwamba Sudan Kusini italipa dola 26 kwa kila pipa la mafuta linalopita kwenye bomba la Sudan,.

    Kupitia mpango huo, Sudani Kusini itasafirisha mapipa 28,000 kupitia Khartoum kila siku.

    Akiongea wakati wa hafla ya utiaji saini, waziri wa petroli wa Sudan Kusini Daniel Awou Chuang alisema makubaliano hayo yanafaidi nchi zote mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako