• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Akinwumi Adesina apigiwa debe kuongoza AfDB kwa muhula wa pili

  (GMT+08:00) 2019-12-31 20:13:43
  Jumuiya ya Uchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) imeidhinisha uwakilishi wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Akinwumi Adesina kwa muhula wa pili katika uongozi wa taasisi hiyo.

  Uamuzi huo ulitangazwa mwishoni mwa kikao cha kawaida cha hamsini na sita cha Mamlaka ya Wakuu wa Nchi na Serikali za nchi za ECOWAS, kilichofanyika huko Abuja, Nigeria.

  ECOWAS ilisema kwa kutambua utendaji mzuri wa Dk. Akinwumi Adesina Mamlaka hiyo inaidhinisha uwakilishi wake kwa muhula wa pili kama Rais wa benki hiyo.

  Adesina ni Rais wa nane aliyechaguliwa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika. Alichaguliwa katika kipindi cha miaka mitano mnamo Mei 28, 2015 na Bodi ya Magavana wa Benki hiyo katika Mikutano yake ya kila mwaka huko Abidjan, Cote d'Ivoire, ambapo mchakato huo wa uchaguzi utafanyika mwaka ujao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako