• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Arturo Vidal aishtaki Barcelona akidai hajalipwa pauni milioni 2 za posho mbalimbali

  (GMT+08:00) 2020-01-01 09:13:39

  Kiungo wa Barcelona, Arturo Vidal, amechukua hatua ya kushangaza dhidi ya klabu yake hiyo. Ameamua kuishtaki akidai hajalipwa pauni milioni 2 za posho mbalimbali. Wanasheria wake wa Chile walipeleka mashtaka mahakamani Disemba 5 wakidai nyota huyo mwenye umri wa miaka 32, alitakiwa kupewa posho mbalimbali baada ya msimu wake wa kwanza Barcelona kufuatia kutua akitokea Bayern Munich. Vidal aliichezea Barcelona mechi 53 msimu uliopita waliposhinda ubingwa wa La Liga na kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Wanasheria wa Vidal wanasema anatakiwa alipwe posho ya pauni milioni 2 kwa kucheza asilimia 60 ya mechi hizo za Barca. Lakini taarifa ya gazeti la Hispania la ABC, inasema madai yake hayo yanapingwa vikali na Barcelona ambao wanadai hakufikisha hata dakika 45 kwa mechi. Wanadai wanasheria wake wametafsiri vibaya vipengele katika mkataba wake. Vidal anaamini alikuwa anadai pauni milioni 3 laki 5 mia sita thelathini na saba lakini alipewa pauni milioni moja laki nne arobaini na sita elfu mia tatu na themanini na nane tu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako