• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • RIADHA: Brigid Kosgei amaliza mwaka kwa kuwa bingwa wa mbio za Corrida International de Sao Silvestre

  (GMT+08:00) 2020-01-01 09:05:54

  Mshika rikodi wa mbio za marathon kwa upande wa wanawake Brigid Kosgei amekuwa bingwa wa mbio za Corrida International de Sao Silvestre kwa kilomita 15 katika mwaka uliomalizika 2019, zilizofanyika jana Jumanne Sao Paulo, Brazil. Mwanariadha huyo anayefanya mazoezi Kapsait, kaunti ya Elgeyo-Marakwet alikuwa kinara mapema kabla ya kushinda mbio kwa dakika 48 na sekunde 56 mbela ya Mkenya mwenzake Sheila Chelangat aliyetumia muda wa dakika 50:10 huku Muethiopia Tisadk Nigus akimaliza kwa dakika 50:12. Pauline Kaveke mwenye medali ya shaba katika nusu marathoni amemaliza wa nne kwa kutumia dakika 50:51 huku Delvine Meringor pia kutoka Kenya akifunga tano bora baada ya kuvuka utepe kwa kutumia dakika 50:51. Kosgei amesema anatumia mbio hizo kujiimarisha kimwili kwani ameanza mazoezi tena hivi karibuni baada ya kupumzika kwa muda mrefu. Kosgei amebainisha kuwa ataendelea na mazoezi katika mwaka huu mpya kwa lengo la kushiriki mbio kubwa za mwezi Aprili na zile za michezo ya Olimpiki ya Japan.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako