• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TENISI: Sharapova aalikwa kushiriki michuano ya kimataifa ya Brisbane

    (GMT+08:00) 2020-01-01 09:07:56

    Mcheza tenisi wa Russia Maria Sharapova atashindana kwenye michuano ya kimataifa ya Brisbane mwezi huu baada ya kupata mwaliko wa kushiriki mashindano hayo. Mchezaji huyo aliyekuwa namba moja duniani mwenye miaka 32 amecheza mechi 15 tu mwaka 2019 kwasababu ya jeraha la muda mrefu la bega. Sharapova ambaye pia ni bingwa mara tano wa Grand Slam mara ya mwisho alicheza katika raundi ya kwanza ya US Open mwezi Agosti. Wengine wanaotarajiwa kushindana kwenye michuano hiyo inayoanza Januari 6 hadi 12 ni bingwa mtetezi Karolina Pliskova, namba moja duniani Ashleigh Barty, Naomi Osaka na Venus Williams. Michuano hiyo inachukuliwa kama ya kupasha misuli moto kwa ajili ya Grand Slam ya kwanza mwaka huu Australian Open huko Melbourne, inayoanza Januari 20. Kutokana na kuwa kwenye nafasi ya 133 duniani Sharapova anahitaji mwaliko wa kuingia moja kwa moja kwenye michuano Australian Open aliyokuwa bingwa mwaka 2008.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako