• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Hotuba ya mwaka mpya ya Rais Xi yapongezwa na wachambuzi wa nje

  (GMT+08:00) 2020-01-01 09:11:01

  Rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba ya salamu za mwaka mpya, ambayo imepongezwa na wachambuzi mbalimbali wa kimataifa.

  Profesa Evaritus Irandu wa chuo Kikuu cha Nairobi amesema hotuba hiyo imeonyesha dhamira kubwa ya China kutokomeza umaskini, kazi ambayo inahitaji juhudi za makusudi kwa jamii nzima.

  Mchumi wa Japan Kyoshi Wanaka amesema njia ya hatua kwa hatua na maendeleo ya pamoja haitengani na njia ya kujiendeleza kwa amani, na mchango wa China kwenye amani ya dunia na maendeleo.

  Profesa Oleg Timofeyev wa Chuo Kikuu cha Urafiki Cha Russia amesema mwaka 2020 utakuwa ni mwaka muhimu katika historia ya China, wakati inatarajia kukamilisha kazi ya ujenzi wa jamii yenye maendeleo ya kati kwa pande zote.

  Profesa Heba Gamal Edin wa sayansi ya siasa katika taasisi ya mipango ya taifa ya Misri, amesema China inatumia vizuri kanuni ya kutoingilia mambo ya ndani na kutafuta matokeo ya kunufaishana, na kusema China ni mshirika wa kuaminika wa nchi za kiarabu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako