• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Chuo kikuu cha Maasai Mara na chuo cha Sayansi cha China chatarajia kujenga kiwanda cha kisasa

  (GMT+08:00) 2020-01-01 09:13:26

  Chuo kikuu cha Maasai Mara kwa ushirikiano na chuo cha Sayansi cha China kinatarajia kujenga kiwanda cha kisasa cha kutengeneza dawa asili kutoka kwa miti maalum. Kwa sasa, zaidi ya miti 210 ya aina mbali mbali yenye manufaa ya kiafya, imepandwa kwenye bustani maalum katika Chuo hicho. Yote haya yamewezeshwa kupitia taasisi ya utafiti ya SAJOREC kwa ufadhili wa serikali ya China. Mwanahabari wetu Tom Wanjala ana taarifa hiyo.

  Katika hotuba yake Rais Xi Jinping wa China kwenye Mkutano wa Ushirikiano kati ya China na Afrika, FOCAC, mwaka wa 2018 kule Beijing, mojawapo ya hoja nane zilizozungumziwa ni ile ya China kusaidia bara la Afrika katika swala la utafiti, sayansi na teknolojia na kuhifadhi mazingira. Ili kuhakikisha hili limeafikiwa, China imekuwa ikishirikiana na Afrika kwa kujenga taasisi za Sayansi na utafiti.

  Katika Chuo Kikuu cha Maasai Mara nchini Kenya, serikali ya China kwa ushirikiano na chuo hicho, walianzisha bustani ya miti ambayo imefanyiwa utafiti na iliyo na uwezo wa kutumiwa katika matibabu ya magonjwa mbali mbali. Profesa Mohammed Abdille ni mkurugenzi mkuu wa bustani hili.

  Chinese Academy of Sciences ni kama wizara, huku China. Ni zaidi ya taasisi 100. Hawa watu ni wa kimataifa. SAJOREC ilianzishwa kuisaidia Afrika kwa masuala ya teknolojia na utafiti. Profesa Abdille anasema kwamba, Kenya ina utajiri wa tamaduni nyingi na miti mingi ambayo wengi hawajui manufaa yake. Hivyo basi, kuanzishwa kwa bustani la utafiti wa miti katika chuo kikuu cha Maasai Mara, kutasaidia sana kutambua manufaa ya baadhi ya miti katika jamii za Kenya.

  Tuna miti mingi ya dawa. Tukiunganishwa na China, tutapata manufaa sana. KInachotia moyo zaidi ni kwamba kuna wakenya ambao tayari wako China kusomea maswala ya utafiti wa sayansi na haswa miti yenye uwezo wa kutumiwa kama dawa asili.

  One month nilikuwa China. Nilipata wakenya 150 katika Chinese Academy of Sciences. Niliwahimiza wajue tamaduni za China. Lazima tushikane mikono. (Moha 3)

  Je, ni vipi mkenya wa kawaida na Afrika kwa jumla itaifaidika na taasisi ya SAJOREC?

  Afrika, sisi ni tajiri sana. SAJOREC itahakikisha kwamba tuna kiwanda cha kutengeneza dawa asili ili kutatua magonjwa sugu kama saratani. (Moha 4)

  Bustani hii ya Maasa Mara ni tawi dogo la taasisi ya SAJOREC, ambayo makao yake makuu ni katika Chuo Kikuu cha Jomo Kenya. Lengo kuu likiwa kufikia mataifa yote barani Afrika. Profesa Robert Gituru ni mwanzilishi wake.

  Tuna vituo nchini Ethiopia, Tanzania, Madagascar na pia tutafungua vingine kote Afrika. Tumewawezesha vijana kutoka mataifa mengi Afrika, kwenda China kusomea sayansi na teknolojia. Baadhi ya wanafunzi wamerejea na wameanza kuisadia jamii.

  Naitwa Elizabeth Kamande.Nimepata ufadhili kupitia SAJOREC. Nilisomea China.

  Kando na utafiti wa miti na kutengeneza dawa za asili kutoka kwenye miti, SAJOREC inapania kutatua swala la njaa nchini Kenya na Barani Afrika kwa ushirikiano na serikali ya China.

  Afrika nzima, kuna shida ya lishe. Njaa imetusumbua sana kwa miaka. SAJOREC ikishirikiana na China, tunaanzisha kiwanda cha kisasa cha ukulima. (Prof Gituru)

  Ni wazi kwamba ushirikiano kati ya China na Kenya katika suala la sayansi, teknolojia na utafiti litawafaa wakenya wengi siku za hivi karibuni.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako