• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Simba yaingia 2020 na salamu kwa Yanga

  (GMT+08:00) 2020-01-01 16:41:33

  Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Simba Sports Club wameukaribisha mwaka wa 2020 kwa kutuma salamu za ushindi kwa watani zao, Yanga, baada ya kuichapa Ndanda FC mabao 2 – 0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. Mabao hayo mawili yaliyofungwa na wachezaji wa kigeni Francis Kahata raia wa Kenya na Deo Kanda wa DRC ndio yalipeleka salamu Jangwani huku yakiifanya Simba kuongeza pengo la pointi 10 kati yake na Yanga. Ushindi huo umekuja siku chache kabla ya mechi kati ya mahasimu hao wa jadi itakayochezwa Januari 4 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kuelekea mechi hiyo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewaonya mashabiki wa timu hizo kwa kuwataka kuwa wastaarabu wakati wote wa mchezo huo. Kamanda wa polisi wa Kanda hiyo Lazaro Mambosasa amesema, wamejipanga kikamilifu kuimarisha ulinzi katika mchezo huo, akiwataka mashabiki watakaokwenda kutazama mchezo huo kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa Amani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako