• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • KMC yawaondoa hofu mashabiki wake

  (GMT+08:00) 2020-01-01 16:41:49

  Licha ya kushuka dimbani mara 13 na kuambulia alama tisa tu na kushika nafasi ya 17 katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, Mwenyekiti wa Bodi ya KMC FC Benjamin Sitta amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo na kuwataka kuamini timu hiyo itarejesha makali yao ya msimu uliopita. Sitta amesema, lengo lao ni kumaliza Ligi hiyo katika nafasi tano za juu, na hilo linawezekana kwa kuwa timu hiyo inacheza vizuri ikiwa ni pamoja na kumiliki mpira kwa asilimia kubwa. Hata hivyo, mwenyekiti huyo amesema haoni haja ya kuboresha kikosi hicho katika dirisha dogo la usajili kwa kuwa waliopo bado wanacheza vizuri.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako