• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Afya ya Kaseja yawatoa hofu mashabiki

  (GMT+08:00) 2020-01-01 16:42:23

  Uongozi wa timu ya KMC umewataka mashabiki wao wasiwe na hofu na mlinda mlango wao namba moja Juma Kaseja ambaye amefanyiwa upasuaji wa goti hivi karibuni. Ofisa Habari wa KMC, Anwar Binde amesema kuwa kwa sasa maendeleo ya Kaseja yanaridhisha hivyo mashabiki wasiwe na wasiwasi. Amesema kwa sasa maendeleo ya Kaseja sio mabaya kwani ameanza kurejea kwenye ubora wake taratibu kabla ya kuungana na wachezaji wenzake kuendelea na majukumu yake ya kila siku. Kaseja aliyejiunga na KMC msimu wa mwaka 2018-19 ilipokuwa chini ya Etienne Ndayiragije kutoka Kagera Sugar, aliukosa mchezo dhidi ya Simba ambao KMC walipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 uwanja wa Uhuru kutokana na kuwa majeruhi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako