• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wapongeza ununuzi kilo 250,000 tumbaku

    (GMT+08:00) 2020-01-01 19:33:31

    Wakulima wa Chama cha Msingi Ngokolo, Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga, wameipongeza kampuni ya Petrobena kwa kununua tumbaku kilo 250,000 iliyokuwa imebaki na kugawa pembejeo za kilimo hicho kwa msimu ujao kwa wakati.

    Akizungumza na vyombo vya habari, Mwenyekiti wa chama hicho Ally Hamisi, amesema wakazi wengi wa Halmashauri ya Ushetu wanategemea kilimo cha tumbaku kwa maisha yao.

    Alisema awali, wakulima wa tumbaku walikuwa wameshakata tamaa ya kuendelea kulima zao hilo baada ya kuona tumbaku ambayo inazalishwa nje ya kilimo cha mkataba inakosa soko na kutaka kujikita kwenye kilimo cha pamba.

    Aidha, Hamisi alisema, Chama cha Msingi Ngokolo kinawanachama hai 295 ambao baada ya kununuliwa kwa tumbaku iliyokuwa imebaki kilo 250,000 na Petrobena, wakulima hao wamelima zaidi ya hekta 220 za tumbaku kwa ajili ya msimu ujao.

    Hamisi aliomba uongozi wa kampuni hiyo kukiruhusu chama hicho kuongeza uzalishaji kutokana na ukubwa wa chama hicho, na kuongeza kuwa msimu ujao wanamatarajio ya kuzalisha kilo 700 ambazo zitakuwa na ubora unaohitajika kwenye soko la dunia.

    Aidha wakulima mkoani Shinyanga wametakiwa kuendelea kulima tumbaku yenye ubora ili kampuni ziendelee kujitokeza kwa wingi kununua tumbaku, na kuongeza kuwa zinapojitokeza kampuni kwa wingi ndivyo mkulima anavyopata faida.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako