• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Hatimaye meli ya mwaka 2020 yang'oa nanga

  (GMT+08:00) 2020-01-01 19:33:56
  Wakenya na wageni wa tabaka mbalimbali wameukaribisha mwaka mpya kwa mbwembwe shughuli nyingi zikiwa ni Pwani ya Kenya na jijini Nairobi.

  Katika Kaunti ya Lamu, wageni na watalii mbalimbali waliukaribisha mwaka mpya wa 2020 kwa mtindo wa aina yake, ambapo wengi walionekana wakijivinjari ndani ya bahari.

  Boti na mashua mbalimbali zilizojaa wakazi na watalii zilionekana zikizunguka baharini ilhali nyingine zikiwa zimetia nanga katikati ya bahari huku zikiwa zimepambwa kwa mataa ya rangi tofautitofauti, hivyo kuleta mvuto wa aina yake.

  Wapenda raha wengine pia waliukaribisha mwaka mpya kwa kumiminika kwenye baa ya aina ya boti inayoelea kwenye Bahari Hindi, kati ya mji wa kale wa Lamu na Shella-almaarufu Floating Bar.

  Baadhi ya waliohojiwa hawakuficha furaha yao kwa kufanikiwa kuvuka mwaka wakiwa hai.

  Wafanya biashara wengi walisema wamepata mafanikio mengi baada ya wateja kumiminika kwa wingi katika Pwani ya Kenya kwa ajili ya kujivinjari.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako