Kaimu fundi mkuu wa Tanesco wilaya hiyo, Peter Mtete leo amesema kuwa malipo waliyoona kwenye mfumo ni Sh3 milioni, hivyo hawataweza kufungua huduma hadi deni lote litakapolipwa.
Ameongeza kuwa wana wateja 1500 kati ya wakazi zaidi ya 35,000 wa mji huo ambao walikuwa wanawatoza Sh7,500 sawa na Sh11,250,000 kwa mwezi, umeme ni Sh9-10 milioni lakini wanashindwa kulipa hata kidogo, wamepandisha gharama hadi Sh12,000 kwa mtu mwenye matumizi madogo ambapo wanaweza kusanya Sh18 mil lakini hakuna mabadiliko.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |